Save 20% off! Join our newsletter and get 20% off right away!

Wachezaji Wenye Magoli Mengi Ligi Kuu Tanzania

Wachezaji Wenye Magoli Mengi Ligi Kuu Tanzania: Mchezaji mwenye Magoli mengi Tanzania, Katika historia ya soka la Tanzania, kumekuwa na wachezaji wengi wenye vipaji vya hali ya juu, lakini mmoja wao anasimama kama mfungaji bora wa muda wote katika Ligi Kuu Tanzania. Hapa tutazungumzia mchezaji huyu na mafanikio yake katika soka.

John Bocco: Mfungaji Bora wa Muda Wote: John Bocco ndiye mchezaji mwenye magoli mengi zaidi katika historia ya Ligi Kuu Tanzania, akiwa na jumla ya magoli 47.

Wachezaji Wenye Magoli Mengi Ligi Kuu Tanzania, Amecheza kwa mafanikio katika vilabu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Simba SC na Azam FC. Uwezo wake wa kufunga magoli umemfanya kuwa kipenzi cha mashabiki na kiongozi katika uwanja wa soka.

Wachezaji Wenye Magoli Mengi Ligi Kuu Tanzania

Ligi Kuu ya Tanzania Bara imekuwa na historia ndefu ya wachezaji mahiri wanaoacha alama kupitia mabao yao. Hapa ni orodha ya wachezaji waliowahi kushikilia rekodi ya kuwa wafungaji bora kwa msimu mmoja, Wachezaji Wenye Magoli Mengi Ligi Kuu Tanzania, wakifunga mabao mengi zaidi kwenye historia ya soka la Tanzania:

1. Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ – Yanga (Mabao 26)

Mohamed Hussein maarufu kama “Mmachinga” ndiye mfungaji bora wa muda wote kwenye historia ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Alifunga mabao 26 msimu wa 1997, akiisaidia Yanga kutwaa ubingwa kwa pointi 44, huku Simba ikimaliza na pointi 38. Katika msimu huo, Yanga ilifunga mabao 30, ambapo mabao manne tu yalifungwa na wachezaji wengine. Rekodi yake ya mabao 26 bado haijavunjwa.

Wachezaji Wenye Magoli Mengi Ligi Kuu Tanzania
Wachezaji Wenye Magoli Mengi Ligi Kuu Tanzania

2. Abdallah Juma – Mtibwa Sugar (Mabao 25)

Mwaka 2005, Abdallah Juma alikaribia kuvunja rekodi ya Mmachinga kwa kufunga mabao 25 akiwa na Mtibwa Sugar. Hata hivyo, timu yake ilimaliza nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi, huku Yanga ikitwaa ubingwa. Licha ya mafanikio binafsi, Juma alibaki na bao moja tu kuifikia rekodi ya Mohamed Hussein.

3. Meddie Kagere – Simba (Mabao 23)

Meddie Kagere, Mnyarwanda aliyekuwa akiichezea Simba, alifunga mabao 23 msimu wa 2018/19 na kuwa mfungaji bora wa msimu huo. Kagere aliisaidia Simba kutwaa ubingwa kwa pointi 93, huku Yanga ikimaliza na pointi 86. Rekodi yake inamfanya ashike nafasi ya tatu kwa wafungaji bora wa muda wote wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

4. Emmanuel Okwi – Simba (Mabao 20)

Mganda Emmanuel Okwi alifunga mabao 20 msimu wa 2017/18 na kuwa mfungaji bora wa msimu huo. Alisaidia Simba kutwaa ubingwa wa msimu huo kwa pointi 69. Okwi anashikilia nafasi ya nne kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote kwenye historia ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

5. John Bocco – Azam FC (Mabao 19)

John Bocco, ambaye kwa sasa anaichezea Simba, aliwahi kuwa mfungaji bora msimu wa 2011/12 akiwa na Azam FC, alipofunga mabao 19. Licha ya mafanikio yake binafsi, timu yake haikuweza kutwaa ubingwa na ilimaliza msimu huo na pointi 56, huku Simba ikitwaa ubingwa kwa pointi 62.

Pendekezo la Mhariri: