Save 20% off! Join our newsletter and get 20% off right away!

Mchezaji Anaelipwa Pesa Nyingi Tanzania 2024

Mchezaji Anaelipwa Pesa Nyingi Tanzania 2024: Wachezaji wanaovuta mkwanja mrefu kwenye ligi kuu Tanzania NBC kwa msimu huu:

Kumekuwa na maswali mengi kuwa yupi ni mchezaji anaelipwa mshahara mkubwa kwenye ligi ya NBC Tanzania, na hii ni baada ya wachezaji wa kigeni kuonyesha utofauti wao na wachezaji wazawa kwenye viwango vyao vya kiucheaji na thamini ya mikataba yao kiujumla.

Baadhi ya wachambuzi wameweka maoni yao juu ya mchezzaji gani anaelipwa mshahara mkubwa na kura nyingi zimeanguka kwenye vilabu vikubwa zaidi Tanzania vya Simba na Yanga licha ya baadhi ya taarifa zikisema kuwa wachezaji wa Azam wanaongoza kwa masilai yao kwenye mikataba ndani ya klabu hiyo.

Mchezaji Anaelipwa Pesa Nyingi Tanzania 2024

Baada ya maoni mengi leo tumekukusanyia taarifa za mchezji gani anaelipwa mshahara mkubwa zaidi kwenye ligi kuu NBC Tanzania kwa mwaka wa 2024. Wachezaji wazawa walioonekana kulipwa mshahara mkubwa zaidi kwenye ligi kuu  ni pamoja na Feitoto anaekadiriwa kuvuta kitita cha shilingi M23 Tsh. Wachezaji wengine ni kama Zibwe JR, Shomari Kapombe, Jonasi Mkude na Dikson Job ambapo wao wanalipwa zaidi ya M10 kwa mwezi.

Kwenye Orodha ya Wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa kwenye Ligi ya Tanzania NBC wengi ni wachezaji wa kutoka nje ya nchi ambao wameonekana na viwango vikubwa na hata thamini yao kwenye soko la mpira ni kubwa.

Mchezaji Anaelipwa Pesa Nyingi Tanzania 2024
Mchezaji Anaelipwa Pesa Nyingi Tanzania 2024

Wachezaji wa kigeni wengi wanalipwa mishahara mizuri kulinganisha na wachezaji wa kizawa wa Tanzania, na hii ni kwasababu ya mchango wao na thamani yao kwenye mikataba. Sababu zingine ambazo zinaweza changia ni pamoja na kuwa na uongozi mzuri unaowasimamia wachezaji hawa kwenye sajili zao.

Miongoni mwa wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa NBC

Aziz KI Stephane — Yanga | Tsh 31 Milioni

Clatous Chama — Yanga SC | Tsh 27.8 Millioni

Fabrice Ngoma — Simba SC | Tsh 26 Million

Djigui Diarra — Yanga SC | Tsh 26 Million

Ayoub Lakred — Simba SC | Tsh 25.2 Million

Feisal Salum — Azam FC | Tsh 23.8 Million

Jhonier Alfonso Blanco Yus — Azam FC | Tsh 20.3 Million

Jonas Mkude — Yanga SC | Tsh 20 Million

Joash Onyango — Dodoma Jiji | Tsh 18.5 Million

Elvis Rupia – Singida Black Stars | Tsh 18 Million

Aishi Salum Manula — Simba SC | Tsh 17.5 Million

Pendekezo la Mhariri: