Jezi Mpya za Yanga za Mashindano ya CAF, Watangaza Kuzindua: Jezi Mpya za Yanga SC Kutangazwa mapema za CAF kwa msimu wa 2024/2025.
Jezi Mpya za Yanga za Mashindano ya CAF, Watangaza Kuzindua
Klabu ya Yanga SC kupitia kwa mwanamitindo na mbunifu wa mavazi wa kampuni ya GSM Sheria Ngowi, ametangaza kuachia jezi mpya za klabu hiyo mapema na kuwaambia mashabiki wa klabu hiyo kutegemea jezi mpya na kwa upekee wanaweza kuaza kuesabu siku tu kuelekea kilele cha uzinduzi wa jezi hizo.
Licha ya kuwataarifu mashabiki na wapenzi wa klabu ya Yanga, Mbunifu huyo wa mavazi ajaweza wazi tarehe wala mwezi wa kuzinduliwa. Ila kwa taarifa zilizotufikia sisi MichezoHQ wanatarajia kuazindua jezi hizo mnamo tarehe 20 ya mwezi octoba.
Msimu huu miongoni mwa jezi zilizo ongoza kupendwa zaidi na mashabiki na wapenzi wa klabu ya Yanga ni ile jezi ya Kijani, ukitofautisha na msimu uliopita wakati jezi pendwa zaidi ilikuwa nyeusi na njano.
Sheria Ngowi amekuwa akitoa jezi zuri na zenye ubora sana licha ya baadhi ya wapenzi na mashabiki wa Yanga kulalamikia gharama za jezi hizo ambazo mara zote zinauzwa kwa Tsh 45,000 mpaka Tsh 40,000. Hivyo wanatamani zishuke gharama ili kila mtanzania aweze kumudu gharama izo.
Pendekezo la Mhariri:
Leave a Reply