Pamba Jiji Yaachana na Kocha Kopunovic na Wasaidizi Wake: Pamba Jiji FC imeamua kuachana na kocha wake, Goran Kopunovic, pamoja na wasaidizi wake Salvatory Edward (kocha msaidizi), Razack Siwa (kocha wa magolikipa), na Cirus Kakooza (kocha wa viungo).
Pamba Jiji Yaachana na Kocha Kopunovic na Wasaidizi Wake
Uongozi wa klabu hiyo umetangaza hatua hiyo leo, huku wakieleza kuwa kwa sasa timu itakuwa chini ya kocha wa timu ya vijana, Mathias Wandiba, wakati utaratibu wa kumpata kocha mpya ukiendelea.
Hatua hii imekuja baada ya tathmini ya mwenendo wa timu katika mashindano, na uongozi umeweka wazi kuwa wanatafuta mbadala atakayeweza kuleta matokeo bora kwa timu hiyo.
Pamba Jiji kwenye NBC Ligi Kuu Tanzania imekuwa timu ambayo haina kiwango kizuri chini ya Kocha Kopunovic kwani katika michezo 7 ya Ligi Kuu haijafanikiwa kupata ushindi kwenye mchezo wowote, na ikiwa ndio timu pekee ambayo haija pata ushindi wa alama 3 kwenye mchezo. Wametoa sare michezo 4 na kupoteza kwenye michezo 3.
Mbali na matokeo hayo Pamba ni miongoni mwa timu zilizofunga magoli machache zaidi kwenye ligi kuu msimu huu wakiwa wamefunga magoli 2 tu kwenye michezo 7 an kuruhusu kufungwa goli 9.
Hivyo kutokana na mwenendo huo uongozi ukaonelea usitishe mkataba na kocha wake mkuu ili kuboresha eneo la benchi la ufundi. Itakumbukwa Pamba Jiji ndio msimu wao wa kwanza tangu warejehe kwenye ligi ya NBC Tanzania, hivyo viongozi hawaitaji kuishusha daraja timu hiyo.
Pendekezo la Mhariri:
Leave a Reply