Timu 10 Zenye Thamani Zaidi Duniani 2024: Thamani za Klabu za Soka Zikifikia Rekodi Mpya: Manchester United na Real Madrid Zaitawala Orodha ya Forbes
Klabu ya Manchester United, yenye thamani ya $6 bilioni (£4.8 bilioni), imeshika nafasi ya pili kwenye orodha ya Forbes ya klabu za soka zenye thamani kubwa zaidi duniani, nyuma ya Real Madrid ya Hispania ambayo ina thamani ya $6.07 bilioni. Kwa mara ya kwanza, klabu mbili za soka zimevunja rekodi ya kuwa na thamani ya juu zaidi ya $6 bilioni.
Thamani ya Manchester United imeongezeka kwa asilimia 30 tangu mwaka jana, ikiendelea kuwa miongoni mwa klabu za soka zenye ushawishi mkubwa zaidi duniani. Real Madrid imeendelea kushika nafasi ya kwanza tangu mwaka 2022, huku ikiongeza thamani yake kwa asilimia 19. Wapinzani wao wakubwa, Barcelona, ambao waliongoza orodha hiyo mwaka 2021, wamepoteza nafasi ya juu na sasa wameshika nafasi ya tatu.
Timu 10 Zenye Thamani Zaidi Duniani 2024
Ni Real Madrid na Manchester United pekee ambazo zimekuwa ndani ya tano bora kila mwaka tangu jarida la Forbes lilipoanza kuchapisha orodha ya timu zenye thamani kubwa zaidi duniani mwaka 2004/Timu 10 Zenye Thamani Zaidi Duniani 2024.
Klabu nyingine za Ligi Kuu ya Uingereza pia zipo katika orodha ya 10 bora. Liverpool, Manchester City, Chelsea, Tottenham Hotspur, na Arsenal zimeingia kwenye orodha hiyo, zikiwakilisha ushawishi mkubwa wa klabu za Uingereza katika soka la kisasa.
Thamani ya Newcastle United pia imepanda kwa kasi ya asilimia 51 hadi $794 milioni, hasa kutokana na ununuzi wao unaoungwa mkono na Saudi Arabia pamoja na kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao, jambo lililoongeza hadhi na thamani ya klabu hiyo.
Pendekezo la Mhariri:
Leave a Reply