Ake Arejea Mazoezini Manchester City Baada ya Kupona Jeraha: Beki wa Manchester City, Nathan Ake, amerejea rasmi kwenye mazoezi ya timu baada ya kupona jeraha lake la hivi karibuni. Mholanzi huyo sasa yupo fiti kwa asilimia 100%, na kuna uwezekano mkubwa kocha Pep Guardiola atamjumuisha kwenye kikosi kitakachomenyana na Wolverhampton wikendi hii.
Jumapili hii, Manchester City watakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Molineux kuikabili Wolverhampton katika muendelezo wa Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League).
Urejeo wa Ake ni habari njema kwa Guardiola ambaye anatarajia kuimarisha safu yake ya ulinzi kwa ajili ya kuhakikisha ushindi katika mchezo huo muhimu. Mashabiki wa City wanasubiri kuona ikiwa beki huyo atapata nafasi ya kuonyesha uwezo wake kwenye uwanja baada ya kurejea kutoka kwenye jeraha.
Pendekezo la Mhariri:
Leave a Reply