Tabora United Wamesitisha Mkataba na Francis Kimanzi: Klabu ya Tabora United imetangaza kusitisha rasmi makubaliano na aliyekuwa kocha wake mkuu Francis Kimanzi pamoja na msaidizi wake Yusuph Chipo, kuanzia leo, Oktoba 21, 2024.
Tabora United Wamesitisha Mkataba na Francis Kimanzi
Uamuzi huu umefikiwa baada ya pande zote mbili kujadiliana, kutokana na mwenendo wa matokeo ambao haukuwa ukiridhisha uongozi wa timu.
Katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo, imeelezwa kuwa sababu kuu ya kuachana na benchi hilo la ufundi ni kushuka kwa kiwango cha timu kwenye michezo yao ya hivi karibuni, jambo ambalo lililazimu uongozi kuchukua hatua za haraka. Ingawa uongozi umeamua kusitisha makubaliano hayo, wametoa shukrani za dhati kwa kocha Kimanzi na Chipo kwa huduma yao wakati wa kuwa na timu hiyo, huku wakiwaombea mafanikio katika kazi zao zijazo nje ya Tabora United.
Hii inamaanisha Tabora United italazimika kufanya mabadiliko ya haraka ili kuhakikisha timu inarejea katika hali ya ushindani, huku uongozi ukitafuta mbadala wa kocha mkuu na msaidizi wake.
TAKWIMU ZA KIMANZI MSIMU HUU
Michezo: 8
Sare: 2
Ushindi: 2
Kupoteza: 4
Magoli ya Kufunga: 7
Magoli ya Kufungwa: 14
Alama: 8
Nafasi kwenye Msimamo wa Ligi: 11
Pendekezo la Mhariri:
Leave a Reply