Save 20% off! Join our newsletter and get 20% off right away!

Tuzo za CAFA 2024 Kufanyika Marrakech Morocco

Tuzo za CAFA 2024 Kufanyika Marrakech Morocco: Tarehe 16 Desemba 2024

Tuzo za CAFA 2024 Kufanyika Marrakech Morocco, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetangaza kwamba Tuzo za CAF za mwaka 2024 (#CAFAwards24) zitafanyika katika jiji la kitalii la Marrakech, Morocco, tarehe 16 Desemba 2024. Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa Morocco kuwa mwenyeji wa hafla hii ya kifahari inayohusisha wachezaji bora wa soka barani Afrika.

Hafla ya mwaka jana ilileta mbwembwe za Afrika na nyota wengi wa soka walihudhuria, hali ambayo inatarajiwa kurudiwa mwaka huu. Wakati wa kuanza kwa sherehe hizi utathibitishwa na CAF katika muda muafaka, lakini maandalizi tayari yanaratibiwa kwa tukio hili muhimu.

Tuzo za CAFA 2024 Kufanyika Marrakech Morocco
Tuzo za CAFA 2024 Kufanyika Marrakech Morocco

Mwaka huu, mashindano ya CAF Awards yanajumuisha kipindi cha kati ya Januari 2024 hadi Oktoba 2024, ambapo wachezaji na timu mbalimbali zilizofanya vizuri zitatambuliwa kwa mafanikio yao. Victor Osimhen, fowadi wa Nigeria, ndiye anayeshikilia taji la Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Afrika kwa upande wa wanaume, huku Asisat Oshoala akishinda tuzo hiyo kwa upande wa wanawake.

CAF Awards 2024 zitatambua uchezaji wa kipekee katika mashindano ya klabu na ya kitaifa, na tuzo ya juu zaidi itakuwa Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Afrika kwa kategoria za wanaume na wanawake. Nyota mbalimbali za soka barani Afrika zitashindana kuwania mataji haya ya kifahari, na tukio hilo linatarajiwa kuwa na hamasa kubwa.

Pendekezo la Mhariri: