Jack Wilshere Katika Mazungumzo na Norwich City ya Kua Kocha Mkuu: Kocha wa timu ya Arsenal chini ya miaka 18, Jack Wilshere, yupo kwenye mazungumzo makubwa na mabosi wa Norwich City ili kuchukua nafasi ya kocha mkuu wa klabu hiyo. Wilshere anatajwa kuwa mrithi wa Narcis Pelach, aliyekuwa kocha mkuu wa Norwich kabla ya kuhamia timu ya Stoke City.
Hii ni fursa nzuri kwa Wilshere, ambaye ameonesha uwezo mkubwa katika kufundisha vijana. Katika msimu wa 2022-23, aliipeleka timu ya vijana ya Arsenal (U20) hadi fainali ya FA Youth Cup, mafanikio ambayo yamevutia klabu kadhaa, ikiwemo Norwich City, ambayo sasa inatafuta kocha mpya.
Iwapo mazungumzo hayo yatakamilika, Wilshere ataingia katika nafasi ya uongozi wa klabu ya ligi kuu ya Uingereza, hatua muhimu katika ukuaji wake wa kiufundi baada ya kustaafu soka akiwa na historia ya kuwa mchezaji mahiri wa Arsenal na timu ya taifa ya England.
Pendekezo la Mhariri:
Leave a Reply