Save 20% off! Join our newsletter and get 20% off right away!

KUFUZU AFCON 2025, Libya Yalaani Nigeria Kugomea Mechi

KUFUZU AFCON 2025, Libya Yalaani Nigeria Kugomea Mechi: Shirikisho la Soka la Libya (LFF) limeelezea masikitiko yake makubwa kufuatia kitendo cha Timu ya Taifa ya Nigeria, “Super Eagles,” kugomea kucheza mechi ya kufuzu AFCON 2025 dhidi ya Libya, iliyokuwa ipigwe jijini Benghazi mnamo Oktoba 15, 2024.

LFF imekosoa hatua hiyo kupitia taarifa rasmi, ikieleza kuwa wanalaani vikali uamuzi wa Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) kususia mchezo huo. Libya inatafuta haki na italinda sifa ya taifa hilo kwa kuchukua hatua za kisheria zinazohitajika dhidi ya Nigeria.

Kitendo hiki kilifuatia hali ya sintofahamu iliyowakumba wachezaji wa Nigeria baada ya ndege yao kutua katika mji wa Al Abraq badala ya Benghazi, kisha kudaiwa kutelekezwa bila huduma muhimu kwa muda mrefu. Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) limesema linafuatilia kwa karibu hali hiyo na inachunguza kwa kina kilichotokea.

KUFUZU AFCON 2025, Libya Yalaani Nigeria Kugomea Mechi
Kikosi cha Nigeria Kikiwa Airport

Mzozo huu unatoa changamoto mpya katika safari ya kufuzu kwa AFCON 2025, huku timu zote zikiwa kwenye presha ya kufanikisha tiketi zao za kushiriki mashindano hayo makubwa barani Afrika.

Pendekezo la Mhariri: