Save 20% off! Join our newsletter and get 20% off right away!

Ndoto za Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025 Zimepungua

Ndoto za Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025 Zimepungua: Ndoto za Taifa Stars Kwenye AFCON 2025 Zazidi Kuteketea Baada ya Kipigo Kutoka DR Congo

Ndoto za Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025 Zimepungua

Tanzania (Taifa Stars) imepata pigo kubwa katika safari yao ya kufuzu kwa AFCON 2025 baada ya kukubali kichapo cha magoli 2-0 dhidi ya DR Congo kwenye Uwanja wa Mkapa. Licha ya matumaini makubwa ya mashabiki wa Tanzania, magoli ya dakika za mwisho kutoka kwa Meschak Elia dakika ya 87 na 90 yaliipa DR Congo ushindi muhimu.

Kwa ushindi huo, DR Congo inaendelea kuongoza Kundi H ikiwa na pointi 12, huku Taifa Stars ikibaki na pointi 4 baada ya michezo minne. Hali hii imefanya nafasi ya Tanzania kufuzu kwa AFCON 2025 kuwa finyu zaidi.

Ndoto za Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025 Zimepungua
Kocha wa Taifa Stars bado anamatumaini ya kufuzu kwenye AFCON kwa michezo miwili iliyobaki kwenye kundi ya Guine na Ethiopia.

Taifa Stars sasa inakabiliwa na mechi mbili ngumu zijazo, dhidi ya Ethiopia mnamo Novemba 10, 2024, ugenini, na mechi ya mwisho dhidi ya Guinea mnamo Novemba 18, 2024, nyumbani. Ushindi katika mechi hizo mbili ni muhimu kama wanataka kufufua matumaini yao ya kushiriki michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Pendekezo la Mhariri: