Raisi Lula Da Silva Apendekeza Kutumia Wachezaji wa Ndani Pekee: Wachezaji wa Brazil, Vinicius, Rodrygo, Raphinha na wengine wanaocheza soka nje ya Taifa hilo huenda wakakosa nafasi ya kulitumikia Taifa hilo baada ya Rais wa wa Brazil, Lula Da Silva kuelezea nia yake ya kutaka kuona wachezaji wanaocheza kwenye Ligi ya ndani tu Nchini humo kuitwa kwenye timu ya Taifa.
Raisi Lula Da Silva Apendekeza Kutumia Wachezaji wa Ndani Pekee
Akizungumza kwenye mahojiano siku moja baada ya Brazil kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Chile kwa magoli kutoka kwa wachezaji wa klabu ya Botafogo iliyopo Rio de Janeiro, Luiz Henrique na Igor Jesus, Rais Da Silva amesema wachezaji waliopo nje ya Brazil hawana ubora kuwazidi wanaocheza Ligi ya ndani.
Da Silva (78) amesema kwa sasa hakuna Garrincha au Romário kati ya wachezaji wanaocheza nje ya Taifa hilo na kudai waliopo ni kundi la vijana wadogo ambao bado sio mastaa.
Da Silva amesema tayari amekutana na rais wa Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) na kupendekeza wazo la kuita wachezaji walio nchini Brazil pekee, jambo ambalo litawaondoa Vinícius, Rodrigo, Militão na Endrick kutoka Real Madrid au Raphinha Barcelona kwenye mipango ya Mabingwa hao mara 5 wa kombe la Dunia.
Pendekezo la Mhariri:
- Viingilio vya Kariakoo Derby 19 October 2024
- Haaland Aweka Rekodi Mpya ya Ufungaji Bora wa Taifa la Norway
- Burundi Yachapwa 4-1 na Burkina Faso Kufuzu AFCON 2025
- Tanzania Yapoteza kwa Goli la Kujifunga Dhidi ya DR Congo
- Washereheshaji wa Usiku wa Tuzo za TMA 2024
- Stars Dhidi ya Congo, Samatta na Kibu Waaza kwenye Kikosi
Leave a Reply