Tanzania Yapoteza kwa Goli la Kujifunga Dhidi ya DR Congo
Tanzania Yapoteza kwa Goli la Kujifunga Dhidi ya DR Congo, Kwenye Mechi ya Kufuzu AFCON 2025. Timu ya Taifa ya Tanzania imepoteza mchezo wa raundi ya tatu wa kufuzu AFCON 2025 kwa kipigo cha 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo), mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Stade des Martyrs, jijini Kinshasa. Bao pekee katika mchezo huo lilitokana na goli la kujifunga la mchezaji wa Taifa Stars, Clement Mzize, katika dakika ya 54.
Licha ya juhudi za Taifa Stars kurejea kwenye mchezo huo, walishindwa kupata goli la kusawazisha. Ushindi huo umeifanya DR Congo kuimarisha nafasi yao kileleni mwa Kundi H, wakiwa na pointi 9 baada ya mechi tatu. Tanzania, yenye pointi 4 baada ya michezo mitatu, inasalia katika nafasi ya pili kwenye kundi hilo.
Matokeo haya yanaifanya Tanzania kulazimika kujipanga upya kwa mchezo wa marudiano dhidi ya DR Congo utakaopigwa Dar es Salaam. Mchezo huo utakuwa muhimu kwa Stars endapo wanataka kuongeza nafasi zao za kufuzu AFCON 2025.
Kwa sasa, Tanzania inahitaji kufanya kazi ya ziada katika mechi zijazo ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kutoka Kundi H, ambapo ushindani unaonekana kuwa mkali.
Pendekezo la Mhariri:
Leave a Reply