Save 20% off! Join our newsletter and get 20% off right away!

Washindi na Mabingwa wa Ngao ya Jamii

Washindi na Mabingwa wa Ngao ya Jamii: Ngao ya jamii simba imechukua mara ngapi, Ngao ya jamii Yanga imechukua mara ngapi, Historia ya Washindi wa Ngao Ya Jamii

Michezo ya Ngao ya Jamii imekuwa moja ya mashindano muhimu katika soka la Tanzania, ikileta pamoja klabu bora zinazoshindana kuashiria mwanzo wa msimu mpya wa ligi. Ngao ya Jamii imeanzishwa kwa lengo la kukuza mshikamano na kuleta furaha kwa mashabiki wa soka nchini. Hapa tunakuletea historia na washindi wa kombe hili tangu kuanzishwa kwake.

Ngao ya Jamii ilianzishwa mwaka 2001, ikianza kwa mchezo wa kukata na shoka kati ya watani wa jadi, Simba na Yanga. Katika mchezo huo wa kwanza, Yanga waliibuka washindi kwa kuifunga Simba 2-1. Mabao ya Yanga yalifungwa na Edibily Lunyamila na Ally Yussuph ‘Tigana’, huku bao pekee la Simba likifungwa na Steven Mapunda ‘Garincha’.

Mashindano haya hayakuchezwa tena kwa miaka kadhaa hadi yaliporejea mwaka 2009. Tangu wakati huo, yameendelea kuwa kipimo cha kuashiria mwanzo wa msimu mpya wa ligi, yakihusisha klabu ambazo zimefanya vizuri katika msimu uliopita wa ligi kuu ya Tanzania.

Washindi na Mabingwa wa Ngao ya Jamii

Tangu kuanzishwa kwa mechi za Ngao ya Jamii kwa ajili ya ufunguzi wa msimu mpya wa mashindano, Yanga ndiyo wametwaa taji hilo mara ya nyingi zaidi (mara nane) wakifuatiwa na Simba ambao wamelitwaa mara saba.

Washindi na Mabingwa wa Ngao ya Jamii
Washindi na Mabingwa wa Ngao ya Jamii

Hawa ndiyo mabingwa wa Ngao ya Jamii tangu mwaka 2001 ilipoanzishwa, licha ya kutochezwa kwa miaka saba mfululizo kuanzia mwaka 2004 hadi 2001.

2001 – Yanga
2009 – Mtibwa
2010 – Yanga
2011 – Simba
2012 – Simba
2013 – Yanga
2014 – Yanga
2015 – Yanga
2016 – Azam
2017 – Simba
2018 – Simba
2019 – Simba
2020 – Simba
2021 – Yanga
2022 – Yanga
2023 – Simba
2024 – Yanga

Pendekezo la Mhariri: